1 Kings 11:41-43

41Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Sulemani, yote aliyoyafanya na hekima aliyoionyesha, je hayakuandikwa yote katika kitabu cha matendo cha Sulemani? 42Sulemani alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. 43Kisha Sulemani akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Copyright information for SwhKC